• Breaking News

  Sep 5, 2016

  Mkuu Wilaya Aamua Kugawa Namba yake Hadharani


  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi amewaasa Waratibu, Maafisa Elimu, na wadau wote wa elimu wa Wilaya ya Kongwa katika semina ya mafunzo yakujiandaa na Mitihani ya darasa la saba, Semina hii imelenga mafunzo ya Uadilifu wanapokwenda kusimamia Mitihani ya Wanafunzi wa Darasa la Saba.


  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alifika mapema saa nne (4) za asubui akiwa kama Mgeni Rasmi alisimama ili kufungua Semina hiyo, DC Ndejembi aliwaasa kwa Kuwa Waadilifu, kwani kila mmoja wetu anapoamua kuwa mwadilifu lazima kazi yake ataifanya kwa Uweredi Mkubwa sana na matunda yake Bora yataonekana tu!


  DC Ndejembi kawaambia wasifanye kazi hiyo yakusimamia uchaguzi kwa Kuwa wameambiwa na watapewa Posho basi wafanye ilimradi tu bora liende. Ndejembi kaawaambia maafisa hao kuwa Kazi yakusimamia mitihani ya Darasa la saba sio ya lelemama kwani tunahitaji kupata vijana safi na makini wenye sifa na sio bora liende.


  Kasema kwa wilaya yake hatopenda kuona anashika mkia kwa Mkoa wa Taifa, anatamani kuona anashika namba moja ama kwenye kumi bora basi Kongwa iwemo, na itawezekana tu kama walimu hao watajituma kwa Uadilifu, Nidhamu na Uzalendo wa hali ya Juu!


  Mbali na hayo DC Kongwa  DC kasema wasijikute wanakuwa watu wakuuza mitihani nakuwapatia vijana hao ili wafanikiwe katika mtihani, kwani wakifanya namna hiyo watakuwa wanaandaa Kundi la Vijana Mbumbu kama sio Vilaza, jambo ambalo ni baya sana kwa Taifa kwani tunapowapa mitihani wanafunzi hao wanafaulu na baadae huko mbele hushindwa kufanya vizuri na matokeo yake tunakuwa tunaandaa Taifa la Mbumbu tu!


  Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kongwa amegawa namba yake ya simu hadhalani lengo kuu nikupata nakupokea Kero, Changamoto na Maoni yoyote yahusuyo Kongwa lakini hasaa kwa kipindi hiki cha Vijana wa Darasa la Saba wanapokwenda kufanya Mitihani yao ya Darasa la Saba, ivo kaomba walimu na maafisa hao waseme kama kuna changamoto ya aina yoyote kwa wakati itatuliwe, lakini waendelee kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu mkubwa ili kujenga Kongwa yenye Mafanikio makubwa kwa Nidhamu Kubwa!


  Mkuu wa wilaya alifungua Semina hiyo na kisha kuwaaga ili kuwapisha wafanye semina yao kwa Uhuru, Semina hiyo inatarajia kuleta mabadiliko makubwa kwa Tasnia ya Elimu kwa kipindi hiki chakuelekea mitihani ya Darasa la saba. 

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku