Sep 28, 2016

Mo Dewji Awatishia Nyau Yanga ‘Lazima Wakae’ Kandambili Mahali Pake ni Uwani

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kupigwa kwa mechi ya wa watani wa jadi, Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya Oktoba mosi, tayari tambo za mashabiki zimeanza.

mohammed-dewji-702x336

Shabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ameandika ujumbe wa utani kwa mashabiki wa Yanga na kuwaambia kuwa siku hiyo watachezea kichapo.

“Yanga lazima wakae, kandambili mahali pake ni uwani. #SimbaNguvuMoja,” aliandika MO.

Hivi karibuni uongozi wa Simba ulikubali kufanya mabadiliko na kumruhusu Dewji kuwekeza kwenye klabu hiyo.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

1 comment:

  1. SIMBA KWAKE NI PORINI,LAZIMA SIMBA AFUKUZWE ARUDI KUNAKOSTAHILI(PORINI)

    ReplyDelete

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR