Sep 8, 2016

Mr Blue: Mke Wangu Akisema ‘Yes’ Hakuna wa Kunibabaisha!

Mr Blue
Mr Blue amesema kwa sasa amekuwa mtu mzima na kwamba mambo ya kupiga pamba kama zamani amewaachia wasanii vijana zaidi.

Akiongea na Clouds Fm, rapper huyo amesema kama mke wake atapenda anachovaa, hakuna kinachompa mawazo tena.

“Unajua unapokuwa pia na mambo nayo yanabadilika, najitahidi sasa hivi navaa simple, lakini nimependeza siwezi tena kuvaa yale manguo sijui makubwa au unikute nimevaa kijinsi sijui kimenibana au kipo kama sketi siwezi,” alisema.

“Na wala huwa sina sijui role model, nikienda dukani hiki kizuri navaa. Mke wangu ambaye ndio nimemuoa akiniambia yeye nimependeza inatosha kabisa, hata kama nimevaa taulo natoka nalo tu mambo ya kwenda na wakati sasa nawaachia wadogo zangu kama akina Young Killer, Jux,” alisisitiza Blue.


Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Tupe Maoni Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com