Winga Mrisho Ngassa amevunja mkataba na timu ya Free State Stars ya Afrika kusini baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano

Ngassa alijiunga na klabu hiyo Mei 2015 ambapo alisajiliwa na kocha Kinnar Phiri na kudondosha wino wa miaka minne kwa sasa mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.

Klabu ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini ilitoa barua ya kuvunjwa mkataba huo na Meneja Mkuu Rantsi Mokena inaonesha mkataba huo umevunjwa tangu August 25, 2016.

Haijulikani mpaka sasa anaelekea wapi


Post a Comment

 
Top