• Breaking News

  Sep 7, 2016

  Msigwa 'Awatolea Uvivu' Mawaziri wa Magufuli!

  Mch Piter Msigwa
  Alichangia mswaada wa haki ya kupata taarifa mbunge wa Iringa mjini Mch Piter Msigwa amesema taifa limesinyaa kwa sababu mawaziri ni waoga wa kumkosoa hata kumshauri rais. " Huu mswaada mbovu ulipita kwenye baraza la mawaziri kwa sababu mnaogopa kumkosoa rais, huyu amekuwa kila kitu na kufungia kila kitu". Aliongeza "Mkileta mswaada kama huu sisi hatuogopigi kumkosoa, ukienda maabara ukaambiwa unaendesha haufungi maabara bali unatafuta tiba".


  "Sasa ninyi mmekuwa waoga mpaka mnatia huruma, na rais wenu hana urafiki atawafurumua huko mje huku back bencher kukutana na sheria mbovu mlizopitisha wenyewe, hamuoni wenzenu mliokuwa nao tumekaa nao huku?" alisema. Amesema anashamshangaa Dr Mwakyembe na usomi wake kutumwa kupotosha sheria ya vyama vya siasa. Hivi wewe Mwakyembe na usomi wako kweli ile ndiyo tafsiri ya sheria ya vyama vya siasa? Kweli? "Eti kuna watu mnachangia eti mnalinganisha Tanzania na nchi za Ulaya kwa demokrasia, sisi tulinganishe na Rwanda"

  Amewataka wabunge wa Ccm kuacha kuamini watatawala milele kwani hata Roma Empire ilianguka. "Hata Lowassa alikuwa huko kwenu, leo tunapigwa naye, tunafungwa naye na maji ya washa washa tunamwagiwa naye"

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku