• Breaking News

  Sep 20, 2016

  MTOTO Azaliwa Wakati Mama yake Akiwa Marehemu Baada ya Kupigwa Risasi

  Mwanamke mmoja mjamzito mkazi wa Chicago, Marekani, ameuwawa kwa kupigwa risasi na kufariki hapo hapo lakini mtoto aliyekuwa tumboni hakudhurika.

  Madaktari jana walimfanyia upasuaji na kufanikiwa kumtoa mtoto huyo wa kike salama na kumpa jina la ‘Miracle’ yaani Miujiza.

  Watu wasiofahamika walimpiga risasi msichana huyo Parasha Beard,(19) juzi, usiku eneo la South Chicago akiwa na mpenzi wake.

  Parasha alikuwa na ujauzito wa miezi sita wakati anapatwa na mauti hayo, lakini madaktari waliweza kumtoa salama mtoto huyo ambaye kwa sasa amewekwa kwenye kifaa cha kulea watoto njiti(Incubator)


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku