• Breaking News

  Sep 21, 2016

  Mwalimu Mkuu Atorokea Dirishani Baada ya Kumnajisi Mtoto Kenya


  Mwalimu mkuu wa shule moja katika kaunti ya Bungoma anatafutwa na polisi baada ya kupatikana akishiriki ngono na msichana wa umri wa miaka 12

  Maafisa wa polisi wanamtafuta mwalimu mkuu katika kaunti ya Bungoma ambaye ameenda mafichoni baada ya kupatikana akifanya mapenzi na msichana wa umri mdogo.

  Samuel Masafu Kongoni , mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Lugusi katika eneo la Webuye, alipatikana afisini mwake akitekeleza kitendo hicho.

  Kongoni anasemekana kumtuma msichana huyo dukani siku ya Jumamosi, Septemba, 17 na aliporudi, mwalimu huyo alifunga mlango wa afisi yake na kumnajisi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku