• Breaking News

  Sep 19, 2016

  MWENYEKITI UVCCM Arusha Afikishwa Mahakamani Kwa Kujifanya Usalama wa Taifa

  Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya leo amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbili za kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa na kugushi kitambulisho cha usalama wa taifa.

  Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa CCM katika Kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha alikamatwa na polisi Septemba 16 na alikaa rumande kwa mahojiano hadi leo alipofikishwa mahakamani.

   Mwendesha mashitaka wa serikali, Lilian Mmasi alieleza mahakama kuwa, Sabaya alitenda kosa la kwanza Agosti 13 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Skyway jijini hapa.

  Alisema alijifanya ni mtumishi wa  Usalama wa Taifa wa kujipatia huduma mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.

  Alisema katika kosa la pili, katika muda usiojulikana, Sabaya anatuhumiwa kugushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa namba MT.86117 wakati akijua ni kosa la jinai kufanya hivyo.

  Baada ya maelezo hayo, Sabaya alikana makosa hayo na wakili wake, Yoyo Asubuhi alimuomba hakimu mkazi  Gwantwa Mwankuga ampatie dhamana mteja wake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku