• Breaking News

  Sep 1, 2016

  Mwenyekiti wa Kijiji Atuhumiwa Kuwauwa Vikongwe Wawili Kwa Tuhuma za Uchawi


  Polisi wamemfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Kijiji cha Chambo, Clement Shija kwa tuhuma za mauaji ya vikongwe wawili kwa imani za ushirikina.

  Awali, mwenyekiti huyo alitoroka baada ya kutokea kwa mauaji hayo, hali iliyosababisha polisi kuendesha msako uliofanikisha kumkamata.

  Akimsomea mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Kenedy Mtembe, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Masatu alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti baada ya mtoto wake kufariki dunia.

  Masatu alidai mshtakiwa baada ya kufiwa na mtoto, aliongoza na mamia ya wanakijiji wenzake kwenda kuwashambulia vikongwe hao kisha kuwateketeza kwa moto.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku