• Breaking News

  Sep 13, 2016

  Mwigulu: Wanaomuita Rais ‘Dikteta’ ni Waliopenda Kupindisha Sheria

  Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amesema rais Dkt. John Pombe Magufuli anafuata sheria na anapenda haki.

  Ameyasema hayo kuwajibu watu wanaoendelea kumuita Rais Magufuli ni dikteta.

  “Rais wetu ni mtu anayeishi kwa kufuata sheria na ni mtu anayependa haki kwahiyo wale wote wanaopenda kupindisha sheria, wanaopenda kutenda uovu wanapokutana na sheria ndio hao utasikia wananungu’nika, wanalialia,” amesema. “Niwaambie tu kwamba kama hawawajui madikteta waende upya wafuatilie dikteta anakuaje, nikwambie hata kwa maeneo ambayo tumewahi kuona yakiwa na viashiria vya kidikteta kwanza mtu kusema tu huyu ni dikteta kwanza anakuwa ashakimbia kwenye hiyo nchi.”

  Aliongeza, “Hapa Tanzania wanaosema hivyo sasa hivi wako na soda zao, wengine wako disko, wengine wako wapi wako na ratiba zao za kila leo, wanafurahia maisha huku wanasema hivyo, utaona utawala wa sheria unaendelea, Rais hajatoa hukumu hata moja, vyombo vinaendelea kufanya kazi, kila chombo kinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria,huo ni utawala wa sheria lakini kwa maeneo yaliyowahi kuwa na madikteta ambao sisi tunawajua. Kuna watu waliwahi kunyongwa uwanja wa taifa na anayesimamia zoezi hilo ni kiongozi yeye mwenyewe yaani hawajapitia hatua hata ya mahakama, yeye mwenyewe kiongozi ndiye anaamuru wanyongwe.”

  Aidha Nchemba alitoa ufafanuzi kwa wale ambao hawajui maana nzima ya udikteta, “Hawa watu ambao hawajui labda dikteta anakuaje wasichanganye udikteta na utawala wa kufuata sheria, huu ni utawala wa kufuata sheria,kwamba mtu anakiuka sheria anakutana na mkono wa sheria,mtu anayefanya makosa anakutana na sheria, na kama unavyoona kila aliyefanya makosa mpaka sasa anafikishwa katika mkono wa sheria, awe amefanya uvunjifu wa mali za umma bila kujali utajiri wake anafikishwa katika mkono wa sheria, huu sio udikteta ni utawala unaosimamia haki za wanyonge, ni utawala unaosimamia sheria inasemaje ukishakiuka sheria uwe tajiri uwe maskini unafika kwenye mkono wa sheria,”, alisisitiza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku