Sep 17, 2016

Naongoza kwa Kutukanwa Kwenye Muziki, Lakini Najivunia Kuupeleka Muziki Sehemu Fulani – Ruge


Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema yeye ni mtu ambaye anaongoza kwa kutukanwa katika tasnia ya muziki kutokana na harakati zake za kuupigania muziki.

Akiongea Ijumaa hii katika semina ya wasanii wachanga wa Dodoma iliyofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Ruge amewataka wasanii hao kuacha kukata tamaa katika harakati wanazopitia.

“Mimi ni mtu ninaeongoza kwa kutukanwa kwenye tasnia ya muziki,” alisema Ruge. “Nimetukanwa sana lakini hilo haliniumizi, najivunia kwa kuwa tumepambana sana kuusimamisha muziki wetu hadi kufika hapa,”.

Ruge Mutahaba ni mmoja kati ya watu waliosaidia kwa namna moja kuchochea kukuwa kwa muziki wa bongofleva nchini licha ya baadhi ya watu kutokubali harakati zake.

Bongo5

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR