• Breaking News

  Sep 6, 2016

  Nape Awataka Wananchi Kuwatenga Wasanii wa Kike Wanaovaa Nguo fupi


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewataka wananchi kuwatenga wasanii wa kike ambao wanavaa nguo ambazo zinaacha sehemu zao za mwili wazi


  Akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mery Mwanjelwa (CCM) Jumanne hii kuhusu ushiriki wa viongozi wa dini pamoja na jamii katika kulinda sanaa ili itumike vizuri bila kumzalilisha mwanamke, Nape amesema kila mtanzania ana haki ya kulinda hadhi ya mwanamke.

  “Wizara yangu inatoa wito siyo tu kwa viongozi wa dini, hawa wasanii wetu wamo katikati ya jamii zetu, hawa wasanii ni watoto wetu, ni ndugu zetu, wanaingia kwenye nyumba mbalimbali za ibada na kukutana na viongozi wetu wa dini, natoa wito kwa kila mmoja wetu aone kwamba kuna umuhimu wa kila mmoja kushiriki na kuwahamasisha wasanii wetu wanazingatia maadili ya Tanzania sana katika shughuli zao za sanaa,” alisema Nape. 

  “Nataka nilihakikishie mbunge lako mweshimiwa spika ikiwa jamii itayakataa matendo yanayofanywa na wasanii, wasanii hawa wataacha haya matendo lakini ikiwa jamii itayashabikia nakuyapenda wasanii hawa wataona ndio fashion na wataendelea kuyafanya kwa hiyo hata kama sisi tukihamasisha namna gani, kama jamii haitayakaa na kuyaona hayafai kila mtanzania ataona mwanamke akidhalilishwa amedhalilishwa mzazi wake, amedhalilishwa ndugu yake, haya matendo yatakoma katika jamii yetu, nadhani ni swala jamii zaidi kuyakataa na kuwatenga kijamii wale ambao wanafanya shughuli za kuwadhalilisha akina mama wetu,”

  Pia Nape alisema mpaka sasa kuna wasanii wawatu wa kike ambao walifungiwa kutokana kufanya shughuli za sanaa kinyume na maadili.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku