Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa Paul Pogba wa Manchester United amelazimika kuwapa moyo mashabiki wake baada ya timu yake kupoteza mechi mbili mfululizo.

Jumapili, Septemba 18 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano wa ligi kuu ya England dhidi ya Watford na kufungwa magoli 3-1. Kiungo huyo wa Ufaransa ambaye hadi kwa sasa hajafanya vizuri kama wengi walivyokuwa wana matarajio akiwa na Man United toka avunje rekodi ya usajili.

Kupitia Instagram, Pogba ameandika: Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, Man United tunaweza.”


Post a Comment

 
Top