Sep 24, 2016

PAUL Pogba Azinduka Usingizini..Aisaidia Man United Kuibuka na Ushindi Dhidi ya Leicester City


Manchester United Jumamosi hii imerudisha furaha kwa mashabiki wake baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya mabingwa watetezi wa Premier League, Leicester Cty.

United ambayo ilikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, Old Trafford ilionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika mabao yote manne huku nahodha wake, Rooney akianzia benchi.

Kwa matokeo haya, United inaongeza alama tatu na hivyo kufikisha jumla ya pointi 12 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo wamefanikiwa kushinda michezo minne, imepoteza miwili na haijatoa sare.

Mabao ya United leo yalifungwa na: Smalling dakika ya 22; Mata (36), Rashford (39), Pogba (42) huku lile la Leicester likiwekwa kimiani na Gray dakika ya 60


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR