Katika mahojiano na sauti ya Amerika VOA Swahili jioni hii, Mwenyekiti aliyejiuzulu wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali na kikao kilichomvua uanachama ni batili.

Akihojiwa na mwandishi wa habari mahiri Sunday Shomari, Mwenyekiti huyo aliyejiuzulu amesisitiza kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali kwa mujibu wa katiba ya CUF na kikao kilichoongozwa na Mhe. Katani huko Unguja ni batili na yeye anaendelea na shughuli za kichama kama kawaida.

Naona mchezo ndo kwanza umeanza.


Post a Comment

 
Top