• Breaking News

  Sep 12, 2016

  Rais Hakushauriwa vyema Ujenzi wa Barabara ya Morocco Mwenge

  Wadau nimepita kwenye hii barabara baada ya ukarabati wake, nalazimika kusema kuwa hakuna tija ya kuijenga kwa namna ilivyo sasa.

  Kwa kipindi ambacho misongamano ya magari inahitaji kupunguzwa ingekuwa vyema sana kama barabara hii ingejengwa kwa namna ile ya Morogoro road kuwezesha basi za haraka kupita na kubeba abiria wengi kutoka Mwenge kuelekea Kariakoo na Posta.

  Licha ya kusaidia abiria wengi zaidi pia ungeongeza tija kwa mradi Wa DarT kwani abiria wengi wangeshawishika kutumia usafiri huu tofauti na sasa ambapo wanategemea gari zinazofika Makumbusho moja kwa moja. Ingekuwa ni sawa na kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku