• Breaking News

  Sep 9, 2016

  Rais Magufuli Amemaliza Kazi, Upinzani Sasa Unatapatapa

  MaJaribio yote ya Wapinzani kumdhoofisha Rais Magufuli yamegonga UKUTA(siyo UKUTA wa CHADEMA)

  1. Rais Magufuli hana matatizo, tatizo ni mfumo uliomo ndani ya CCM. Ushahidi kuwa Magu kaushinda mfumo uliokuwa unasema nao ni pale weneyewe waliposema "WANAOISOMA NAMBA SASA NI CCM WENYEWE". Hoja hiyo imekufa.
  2. Magufuli alipoanza kazi ya utumbuaji majipu wakasema wenyewe, kwamba anatekeleza ilani ya Upinzani ya kupigana vita ya rushwa na uzembe kazini. Ushahidi wa kwamba Magufuli anatekeleza ilani ya CCM ni kauli zao wenyewe kwa nyakati tofauti: wafanyabiashara waliochangia CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wanaonewa, Wafanyakazi wanafukuzwa kazi bila kupewa nafasi ya kujitetea, wanahoji kwanini wafanyakazi waliosimamishwa kazi bado wanalipwa mishahara kwa nini? wanasahau kuwa walisema wanaonewa n.k
  3. Baada ya kuona Upinzani unatoweka machoni na masikioni mwa Watanzania kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza dhana nzima ya HAPAKAZITU kwa vitendo, wakaja na maneno chungu nzima , hoja ya msingi ambayo hata mimi nilion ni SIASA NI AJIRA wakiwa na maana kwamba wasipofanya siasa watakufa njaa. Kutaka kuhalalisha hoja yao ya SIASA NI AJIRA na kwa kutaka kuondokana na aibu hiyo ya kulilia ajira ya kufanya siasa wakaja na porojo kwamba rais ni Dikteta. Ndipo wakaamua KUJISHIKISHA UKUTA ambao hata hivyo wananchi walipuuza na kuwafanya wakimbilie KUBADILI GIA angani kwamba wameombwa na Viongozi wa dini na wadau wengine wasitishe hadi Oktoba mosi. Taarifa zlizopo ni kwamba MBowe alitangaza kusitisha UKUTA siku moja kabla ya siku ambayo Viongozi wa dini walipanga kukutana kutoa tamko la kulaani UKUTA. Mpaka leo hakuna MDAU wa KIONGOZI wa dini amejitokeza kusema ni kweli walikutana na Mbowe kuomba wasitishe UKUTA zadi ya tamko la Mwenyekiti wa NCCR Mageuz, James Mbatia kuwa Viongozi wa dini waliwaomba Wabunge wa UKUTA warudi Bungeni, Ombi la Wabunge wa UKAWA kurudi Bungeni na UKUTA wapi na wapi? wanatapatapa tu.
  4. Sasa kinachofanyika ni kuwatumia watu mbalimbali ndani na nje ya nchi kuwashambulia viongozi wa serikali na serikali za yake, kuzusha mambo ya uongo dhidi ya serkali, kutumia maneno ya upotoshaji kwa wananchi. Mfano ni uzushi wa kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi nyingine kama vile kenye, kutokuwepo wa mahusiano mzuri baina ya viongozi wetu wa kitaifa. Mbaya kabisa upotoshaji huu umekwenda mapaka Bungeni, Mbunge anasimama na kusema kila mtanzania anadaiwa kiasi fulani cha fedha(HONGERA sana kwa Waziri Wa Mambo ya ndani kwa kuwaweka bayana Watanzania kuhusu hilo).
  Mambo mengi Wapinzani watayasema kuhusiana na serikali ya awamu ya tano, lakini bahati nzuri wenyewe wanjaua Wananchi wanajua na Dunia inajua kuwa porojo, Propaganda, Uzushi, Matusi, fedheha na dhihaka kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dr. John Pombe Magufuli ni jitihada zao tu za kuifanya SIASA IONEKANE NI AJIRA kwani bila mbinu hiyo watapotea ndiyo maana WANATAPATAPA.
  WATANZANIA TUFUNGUE MACHO, TUTEGE MASIKIO, TUNUSE, TUZIFANYE NGOZI ZETU ZIHISI HAWA MAADUI AMBAO WANATAKA KUWATUMIA HAWA WANASIASA KUDHOOFISHA HIZI JUHUDI ZA MAGUFULI.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku