• Breaking News

  Sep 27, 2016

  RAIS Magufuli Awapa Mtihani Mzito Bandari ya Dar

  Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametoa miezi miwili kwa wafanyakazi wa bandari jijini Dar es Salaam kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini.Ametoa kauli hiyo Jumatatu hii alipotembelea bandari hiyo na kuzungumza na wafanyakazi.

  Ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo ni mbili tu ndiyo zinazofanya kazi na zina uwezo wa kugagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari na kusababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakiki wa udanganyifu.

  “TPA sasa hivi wana bilioni 100 nasema uongo bana,mna bilioni ngapi na bilioni 127, bilioni 40 mtakwenda kununua scanner 10, nataka ndani ya miezi miwili nikute kuna scanner hapa zaidi ya nne zinazofanya kazi, kwahiyo mkagoogle, mkafanye nini, mnunue scanner zifanye kazi”, alisema Dkt Magufuli.

  “Na mjipange angalau kwa kipindi cha miezi mitano lazima tuwe na scanner zaidi ya sita hapa na hizo scanner zisije zinakuwa operated na mtu mmoja, nataka TRA muwepo,TPA muwepo na vyombo vya usalama,” aliongeza.

  Pia Magufuli alisisitiza ulazima wa kufanyika ukaguzi wa vyeti vya wafanyakazi wa bandari hiyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku