• Breaking News

  Sep 19, 2016

  RAIS Magufuli: Kagera Wanahitaji Misaada sio Maneno

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka wanasiasa nchini kutotumia kisiasa maafa ya Kagera yaliyotokana na tetemeko la ardhi.

  Alitoa kauli hiyo hivi karibuni Ikulu jijini Dar es Salaam wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimpa taarifa ya maafa yaliyotokana na tetemeko la ardhi huku akiwataka wanasiasa nchini kutotumia maafa hayo kisiasa.

  “Hii ni mipango ya Mungu,tetemeko haliletwi na serikali, wala tetemeko haliletwi na CCM,ni jukumu la sasa hivi sisi kama nchi, ni kuhakikisha tunawasaidia wenzetu ambao wamepata matatizo hayo, tusilitumie tetemeko hili kwa kujiimarisha kisiasa,” alionya. “Watu wa Kagera wanahitaji misaada sio maneno,” alisema Rais Magufuli.

  Aidha litoa onyo kwa watu wote wasiokuwa na mapenzi mema wanaotumia maafa hayo kukusanya fedha kutoka kwa watu mbalimbali na kutaka vyombo vya dola kuingia kazini.

  “Matapeli wapo na wamejipanga kweli, tunachangia Kagera tunafanya nini, kumbe anachangia tumbo lake, hili ni lazima tuliangalie, na nitoe wito kwa vyombo vya dola,muwafuatilie hawa, ambao wamekuwa wanasingizia wanachangia Kagera na nini wakati wanajichangia wao. Washikwe ikiwezekana wapelekwe kwenye vyombo vya sheria,ili wakajibu hizo hoja za kitapeli na wizi wa kuwaibia watu maskini wenye shida za kiukweli ukweli,” alisisitiza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku