• Breaking News

  Sep 3, 2016

  RAIS Magufuli: Kuchezea Amani ni Kucheza Mchezo Usioweza Kuucheza

  Rais Magufuli
  Rais Dkt John Magufuli amewataka wananchi kisiwani Pemba kuondoa tofauti zao za kiitikadi na kushirikiana katika kuijenga Pemba yenye amani, umoja, maendeleo ya kuichumi na ustawi wa jamii.

  Ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Bambani ya kale kati ya mikoa miwili ya Pemba na kuwashukuru wananchi kumchagua kuwa rais katika uchaguzi mkuu uliopita.

  Aidha Dk Magufuli amesisitiza kudumisha amani na kusema serikali yake haitawavumilia watakaoivunja.

  “Mtu atakapojaribu kuchezea amani nataka nikuhakikishie mheshimiwa raisi,atacheza mchezo ambao hata yeye hajui hata namna ya kuucheza, ni lazima tufike mahali watanzania tuambizane ukweli, watanzania wamechoka na gilba za ovyo ovyo, watanzania wanahitaji maendeleo, watazanzania wanataka kwenda mbele,” alisema.

  Kuhusu dhana ya maendeleo, Rais Magufuli alisema, “Mimi maendeleo katika definition ninayoijua, hayana chama, uwe CUF unahitaji maendeleo, uwe CCM unahitaji maendeleo,uwe CHADEMA unahitaji maendeleo,hata ukiwa huna chama unahitaji maendeleo.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku