• Breaking News

  Sep 13, 2016

  SANAMU la Rais Mugabe Lazua Mjadala...Aliyelichonga Ajitetea

  Aliyetengeneza sanamu ya Rais Mugabe asema hakulenga kumkejeli Rais huyo baada ya sanamu hiyo kukosolewa mitandaoni kuwa ni tofauti na sura halisi ya Rais Mugabe..

  Baadhi ya raia nchini Zimbabwe hata hivyo hawajapendezwa na sanamu hizo na wanasema zinaonekana kama vibonzo.
  "Robert Mugabe ametukanwa kwa sanamu hii na bado hajaelewa," mmiliki wa gazeti ambaye pia ni mwanaharakati Trevor Ncube ameandika kwenye Twitter.
  "Ningelikuwa Robert Mugabe yule mtawala wa kiimla, ningeamuru (Benhura) akamatwe na niue sanamu hizo."

  Msanii huyo, ambaye anasema ilimchukua miezi sita kutengeneza sanamu hizo za Bw Mugabe, pia amejitetea.
  "Nilipokea wajibu huu na nikafanya kadiri ya uwezo wangu. Kawaida, kazi yangu si kutengeneza picha (kazi za Sanaa) za kuashiria sura za watu. Bila shaka, hazikutokea kama wengi walivyotarajia," Benhura ameambia shirika la habari la AFP.


  Je Unaona Hilo Sanamu Limefanana na Mugabe?

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku