• Breaking News

  Sep 13, 2016

  Serikali Kufanyia Tathimini Mishahara ya Watumishi


  Serikali imesema kuwa bado inaendelea na tathimini ya kazi kwa watumishi wa umma na punde itakapokamilika, itapanga mishahara na motisha upya kwa watumishi wote wa umma wakiwemo wa sekta ya afya.

  Waziri wa nchini Ofisi ya rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki.
  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki ambapo amesema lengo la kuongeza mishahara na motisha ni pamoja na kuwajengea mazingira mazuri ya kuwahudumia wananchi na kwa weledi na uadilifu.

  Mhe. Kairuki kwa mwaka 2016/2017, sekta ya afya ndiyo iliyoongezewa mshahara kwa kiwango kikubwa kushindwa watumishi walioko serikali kuu na walimu hali ambayo imelenga kuboresha zaidi sekta ya afya na kuondokana na vifo visivyo vya lazima.

  Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wataalamu wa afya na watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia viapo na maadili ya kazi zao na kusema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa kadri ya uwezo wake wa kulipa utakavyoimarika

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku