Sep 7, 2016

Serikali: Marufuku Kutoza Ada za Chuo Kwa Dola

Serikali imevikataza vyuo binafsi vya Tanzania kutoza ada wanafunzi kwa fedha za kigeni.

Agizo hilo limetolewa Jumatano hii na Wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na mafunzo ya ufundi.

Alikuwa akijibu swali la Juma Othumani Hija, Mbunge wa Tumbati lililohoji: Je, serikali inachukua hatua gani kukomesha tabia ya baadhi ya vyuo kutoza ada kwa kutumia fedha za kigeni”

Akijibu swali hilo, naibu waziri, Mhandisi Stella Manyanya alisema:

“Miaka ya nyuma yalikuwepo malalamiko baadhi ya vyuo vya binafsi kutoza ada kwa fedha za kigeni. Kifungu cha (48)1 cha kanuni zinazosimamia utoaji wa elimu katika vyuo vikuu yaani the university general regulation cha mwaka 2013 kinakataza kuwatoza wanafunzi wa kitanzania kulipa fedha za kigeni. Vyuo vinaruhusiwa kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wasio raia wa kitanzania, kama inavyobainisha katika kifungu cha (48)2 cha kanuni tajwa.”

“Kwa misingi hiyo napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wamiliki wa vyuo binafsi kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kupewa onyo kuvifungia na kutoruhusiwa kudaili wanafunzi,” aliongeza.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR