• Breaking News

  Sep 9, 2016

  Serikali Punguzeni Kodi za Magari Watanzania Tutakwisha


  Watanzania wengi sasa hivi wanatumia magari kama vox noah virtz subaru alteza ist kwasababu ya unafuu wa kuzinunua lakini ukweli hizi gari zimekuwa machinjio ya watanzania. Hizi gari hazina chesis ikipiga mzinga inakunjamana kama gazeti mliomo hamtoki lazima mfie humohumo.

  Tofauti na magari kama Land cruiser Landrover Mercedez Benz BMW hizi zinachesis yaani mhimili mkubwa wa chuma kwa chini ambapo gari linakuwa limefungwa gari hili likianguka halikunjamani kutokana na huo uimara wa chesis. Fikiria Dr.Mwakyembe, prof.safari mh.Jafo wangekuwa kwenye noah wangepona kweli?

  Cha ajabu kadi za haya magari ziko juu mno, ushuru wa chini wa hizi gari ni mil 15 hatakama utaileta haina magurudumu, hatakama umeinunua dola mia, ukileta mpya ndio utashika adabu. Fikiria ushuru wa discover4 haupungui mil23 bila kujali umeinunua shs ngapi.

  Ukweli gari sio anasa ndio maana wabunge wakifika tu bungeni anapewa hela ya gari, sasa iwenje mfanyabiashara au mtumishi wa kawaida iwe anasa kwake?

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku