• Breaking News

  Sep 15, 2016

  Serikali Yaendelea na Zoezi la Kuvitambua Viwanda Vilivyobinafsishwa

  Serikali inatekeleza agizo la Rais Dkt John Magufuli la kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi.

  Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Charles Mwijage, ametoa taarifa hiyo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Manyoni, Yahaya Masare, liloelekeza utekelezaji wa rais kuvirudisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kutokufanya kazi tena.

  “Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara na uwekezaji inaendelea na zoezi la kutambua mikataba ya mauzo kwa viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo ama havifanyi kazi vizuri au vimesimamisha uzalishaji kabisa,” alisema.

  “Timu ya wataalamu kutoka katika wizara ya viwanda na ofisi ya usajili wa hazina walifuatiliwa na kufanya tathmini kwa kutembea kiwanda hadi kiwanda hatua ambayo inasaidia kutatua matatizo yaliyopekea kiwanda kutofanya kazi,”aliongeza.

  “Katika uchambuzi wa viwanda vya mikataba hivyo unafanyika kwa ushirikiano wa ofisi ya msajili wa hazina pamoja na wizara za kisekta ikiwemo wizara ya maliasili na utalii, wizara ya nishati na madini,pamoja na wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi.”

  Waziri Mwijage aliongeza kuwa tayari serikali imekitwaa kiwanda cha chai kilichopo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambapo mwekezaji alikiuka makubaliano ya mkataba.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku