• Breaking News

  Sep 26, 2016

  SERIKALI Yaijibu Marekani...Yakataaa Mapendekezo yaliyotolewa na UN


  Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema Serikali imekataa mapendekezo 72 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar.

  Tamko hilo amelitoa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR), ikiwa ni siku chache baada ya Marekani kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa inashindwa kuheshimu haki za binadamu na kulinda utawala wa demokrasia.

  Profesa Mchome amesema Serikali imekataa mapendekezo 72, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130.

  Amesema Serikali imekataa pendekezo la Zanzibar kwa sababu limetokana na msingi kwamba Zanzibar hakuna Serikali ya uwakilishi na ya kidemokrasia.

  Tathmini ya Profesa Mchome haizungumzii suala la kufutwa kwa mikutano na maandamano ya kisiasa, kukamatwa kwa wanasiasa na kuminywa kwa demokrasia kulikosababisha mvutano kati ya Serikali na vyama vya upinzani, na hasa Chadema.

  Profesa Mchome amezungumzia suala la Sheria ya Makosa ya Mtandaoni akisema haiwezi kuchukua mapendekezo hayo kwa kuwa tayari kuna watu wamefungua kesi mahakamani kuipinga, hivyo inasubiri suala hilo liishe.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku