• Breaking News

  Sep 9, 2016

  Spika Ndugai Awaonya Upinzani Wasifukuze Wabunge, Awataka Wajifunze Kutoka CCM

  Spika wa Bunge Job Ndungai
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Jana aliwaonya viongozi wa vyama vya upinzani waache tabia yao ya usultani kufukuza uanachama wabunge wanaotofaitiana nao. Amesema hayo huku akiwakumbusha Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na kama akifukuzwa uanachama basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge na kuwakosesha uwakilishi wananchi.

  Amewaasa wajifunzi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jinsi wanavyoshughulikia nidhamu za wabunge wao ambao wanaenda kinyume na maamuzi ya chama. Ni CCM pekee ambayo haijawahi kumvua mbunge uanachama kwa kutofautiana na Uongozi. Hivi majuzi CUF imewafutia uanachama wabunge wake Sakaya na Maftah,katika Bunge lililopita Hqamad Rashid alifutwa uanachama akaelekea mahakamani, CHADEMA walimfukuza Zitto Kabwe na NCCR-Mageuzi walimfutia uanachama David Kafulila kabla ya kufanya usuluhishi.

  Ndugai katoa somo na kwa tabia hii ni dhahiri viongozi wa vyama vya upinzani hawataki kukosolewa,wanakumbatia usultani na ufalme.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku