• Breaking News

  Sep 19, 2016

  TETEMEKO Lawalaza Mapadri Kwenye Magari Bukoba

  Mapadri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kashozi, Jimbo la Bukoba wanalala kwenye magari baada ya nyumba walizokuwa wakiishi kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea wiki iliyopita.

  Magari hayo mawili ambayo baada ya shughuli za kutwa huegeshwa kando ya nyumba zilizoharibika, yanatumiwa na mapadri wanne kulala huku wafanyakazi wengine wakipata hifadhi kwenye majengo machache yaliyonusurika.

  Akizungumzia adha hiyo, Paroko wa Kanisa hilo, Padri Philbert Mutalemwa alisema tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi na kuharibu kanisa la kihistoria la Kashozi na nyumba za mapadri, wao waliamua kulala kwenye magari.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku