• Breaking News

  Sep 20, 2016

  UCHUMI wa Tanzania Unaelekea Wapi? Mauzo DSE Yashuka Kwa Asilimia 81. Haijawahi Kutokea

  Mauzo katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka Sh 9 bilioni mpaka kufikia Sh 1.7 bilioni kutokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa kufikia Sh 340,000 kwa wiki hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ofisa mwandamizi wa masoko wa DSE, Mary Kinabo amesema kuwa mauzo hayo yameshuka kutokana na ukubwa wa mtaji wa soko kushuka kwa asilimia 2.79 kutoka Sh 21.3 trilioni kufikia Sh 20.7 trilioni.

  Mary amesema kuwa ukubwa wa mtaji kutoka kampuni za ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha Sh 8.2 trilioni kutoka wiki iliyopita.

  Chanzo: Mwananchi

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku