• Breaking News

  Sep 26, 2016

  UTANI wa Zitto Kabwe baada ya Yanga kufungwa na Stand United

  Utani ni moja kati ya vitu vinavyochukua nafasi katika soka na siku zote kama ni shabiki wa soka au mfuatiliaji wa soka, najua utakuwa umewahi kukutana na mashabiki wale ambao hata timu zao wanazozishabikia zikifungwa huwa hawakosi visingizio.


  Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ni moja kati ya mashabiki wa soka waliotumia social network zao kuwatania Yanga baada ya kufungwa goli 1-0 na Stand United, Zitto ni shabiki wa Simba licha ya kuwa wabunge wa Simba walifungwa goli 5-2 na wabunge wa Yanga katumia account yake ya twitter kuwatania watani zao Yanga kwa kupoteza mchezo.

  Kama ulifikiria labda Zitto hatowatania Yanga kutokana na timu yake ya wabunge wa Simba kufungwa na wabunge wa Yanga, utakuwa unakosea bado hakuacha kuwatania kupitia twitter accout yake, tweet tatu za Zitto Kabwe zinazowatania Yanga kufungwa na Stand licha ya kuwa wabunge wa Yanga wamewafunga timu ya wabunge wa Simba kwa goli 5-2.
  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku