• Breaking News

  Sep 24, 2016

  VIDEO: Mapokezi ya Prof. Lipumba Makao Makuu ya CUF

  Baada ya upembuzi Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Mutungi alitoa mwongozo kuwa Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho aidha baadhi ya viongozi na wanachama waliokuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa, Jaji mutungi amesema ni wanachama halali.

  Baada ya tamko hilo la Jaji Mutungi Leo September 24 2016, baadhi ya wanachama wamemsindikiza Prof. Lipumba mpaka makao makuu ya chama hicho yaliyopo buguruni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi ofisi kama mwenyekiti wa halali wa chama hicho.

  Baada ya wanachama kufika eneo zilipo ofisi hizo geti lilikuwa limefungwa na walinzi hivyo iliwabidi kuruka ili kulifungua kwa ndani na baada ya kuingia ofisini Prof Lipumba ameyazungumza haya.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku