Wakati vifo vya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba mikoa ya kanda ziwa juzi ikiongezeka na kufikia 16, baadhi ya mashuhuda wamesimulia tetemeko hilo lilivyokuwa huku wakisema lilidumu kwa muda wa sekunde 30.

September 12 2016 kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV,  Ceaser Redemptius amezungumza na shuhuda wa tetemeko ambaye alishuhudia mama mmoja aliyefariki wakati akiwa kwenye jitihada za kujiokoa kutoka nje ya nyumba bahati mbaya akawa ameangukiwa na sehemu ya Kenopi na kufariki.

"Nilitoka mara moja nikakimbia kutoka ndani nikaruka nje na yule mama akawa amenifuata lakini mama yule hakuwahi kutoka akawa ameangukiwa na kenopi ya nyumba‘:-ShuhudaPost a Comment

 
Top