• Breaking News

  Sep 16, 2016

  Vigezo vya Udahili Kwa Wenye Stashahada Vyashushwa

  Serikali imeshusha vigezo vya udahili kwa ajili ya kujiunga na vyuo vikuu katika mwaka wa masomo 2016/17 kwa waombaji wanaotumia sifa mbadala (Equivalent Qualification) ambao ni wenye Stashahada pamoja na FTC.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kigezo cha ufaulu kwa waombaji wenye sifa ya stashahada (Diploma) kimeshushwa kutoka GPA ya 3.5 hadi GPA ya 3.0, ili kutoa nafasi kwa waombaji wengi zaidi kupata nafasi katika vyuo mbalimbali.

  Taarifa hiyo pia imeshusha kigezo kwa waombaji wenye Full Technician Certificate (FTC) kutoka wastani wa B hadi wastani wa C.

  TCU imewatangazia wote wanaohitaji kuendelea na vyuo vikuu wenye GPA ya 3.0 kwa Stashahada na wastani wa C kwa wenye FTC watume maombi kupitia TCU kabla ya Septemba 23, mwaka huu.
  Pia TCU imesema kuwa wale ambao walikuwa tayari wamekwishatuma maombi, na wanakidhi vigezo hivi hawatakiwi kuomba tena.

  Taarifa hiyo ya TCU haijaweka wazi sababu za mabadiliko haya, ingawa tangu kutangazwa kwa sifa mpya Julai 11 mwaka huu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wakitaka vigezo hivyo vilegezwe.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku