• Breaking News

  Sep 14, 2016

  Viongozi Wanaotumia Madaraka Vibaya Waonywa

  Waziri wa nchi,ofisi ya rais,utumishi na utawala bora, Angella Kairuki, amesema serikali haitamfumbia macho mtu yeyote atakayekuwa kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi na kutumia madaraka vibaya.

  Amesema hayo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuapisha wakurugenzi 13 wa halmashauri walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

  “Wako wakurugenzi wengine wanawatumia watendaji wa vijiji, watendaji wa kata na maafisa tarafa kuwafanyia miradi yao,wako ambao wamekuwa wakijipatia mashamba katika sehemu mbalimbali vijiji, na wamekuwa wakiwatumia hao watumishi wa serikali kuwasimamia kufanya shughuli zao, niseme tu kwamba serikali haitamfumbia macho yeyote atakayetumia madaraka yake vibaya,” alionya Bi. Kairuki.

  Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikipiga vita watu wanaotumia madaraka vibaya ikiwa ni pamoja na kuweka matabaka kati ya viongozi na wananchi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku