• Breaking News

  Sep 16, 2016

  Wasanii wa Fiesta Wachangia Shilingi Milioni 40 Kwa Wahanga wa Tetemeko Bukoba

  Wasanii wanaoshiriki kwenye tamasha la Fiesta, wamechangia shilingi milioni 40 kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na kuharibu makazi ya maelfu ya wananchi hususan mkoani Kagera.

  Wasanii hao Ijumaa hii walitembelea bungeni Dodoma na Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson, kutangaza mchango wao.

  “Asanteni sana vijana wetu na wasanii wetu kwa zoezi mlilokuja kufanya leo lakini pia kwa mchango wenu kwaajili ya maafa ambayo yametupata kama taifa,” alisema Dkt Ackson.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku