• Breaking News

  Sep 23, 2016

  WAZIRI Mbarawa Aionya Bodi Mpya ya ATCL

  Profesa Makame Mbarawa 
  Waziri Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hatasita kuivunja bodi mpya ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) endapo haitafanya mabadiliko yenye tija sanjari na kwenda kasi katika kuleta mafanikio kwa taifa.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari Mbarawa alisema Serikali hairidhishwi na utendaji wa shirika hilo katika kutoa huduma kwa sasa ndio sababu ya kuundwa kwa bodi hiyo.

  "Matatizo ya shirika sio ndege tu ndio maana tumeanza na kubadili uongozi wa juu na kununua ndege mbili ili kuhakikisha kuhakikisha shirika hilo linaanza kwa upyakatika kuhudumia wananchi" amesema.

  Ameitaka bodi hiyo kuhakikishaina fanya kazi kwa umakini na kudhibiti aina yoyote ya ubadhirifu na upotevu wa mapato.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku