• Breaking News

  Sep 7, 2016

  Wenye Vyeti Feki Watakiwa Kujisalimisha

  Baraza la Mitihani nchini Tanzania limetoa msisitizo kwa watumishi wa umma na wasiokuwa wa umma wanaotumia vyeti vya kughushi au vya watu wengine kujisalimisha kabla hawajafikiwa na mkoni wa sheria.

  Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani la Tanzania Dkt. Charles Msonde amesema katika zoezi linaloendelea nchi nzima wamekamata watu wengi ambao ni watumishi wa umma wakiwa wameajiriwa hali ya kuwa wanatumia vyeti ambavyo sio halali ama vya mtu mwingine.

  Dkt. Msonde ametumia fursa hiyo kuwataka watu wengine ambao wanajua wanafanya hivyo kujisalimisha kujitoa wenyewe katika ajira badala ya kusubiri kuumbuliwa na serikali huku akisisitiza wanafanya utaratibu wa kufuatilia suala katika taasisi nyingine ambazo sio za umma wala za kiserikali.
  Katika hatua nyingine wakati wanafunzi wa Darasa la Saba wakiendelea na mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu shule ya msingi baraza la mitihani leo limezitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri zisibweteke kwa kuwa kuna kila dalili ya kutokea udanganyifu katika mitihani hiyo.

  Msonde amesema licha ya matukio ya udanganyifu kupungua lakini endapo itatokea basi wasimamizi watawajibishwa huku akisisitiza hawatasita kufuta matokeo yote endapo udanganyifu utajitokeza kwa kiwango kikubwa.

  Dkt. Msonde amesema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu wa kuundwa kwa kamati za usimamizi wa mitihani za mikoa na Halmshauri matukio hayo ya udanganyifu yamepungua kabisa kulikopeleka mpaka matokea ya mwaka jana kuwa hakuna hata kisa kimoja cha udanganyifu.

  Katibu mtendaji huyo amezitaka kamati hizo kutoa taarifa haraka pindi watakapobaini hali hiyo ya udanganyifu ili hatua za haraka zichukuliwe ikiwa ni lengo la kutoa wanafunzi wenye sifa watakaoendelea na elimu ya sekondari.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku