• Breaking News

  Oct 10, 2016

  ACT Wazalendo Waazimia Mambo 3, Katiba, Gesi Vimetajwa


  CHAMA cha ACT Wazalendo kimemaliza Mkutano wake wa kwanza wa kisera tangu uchaguzi Mkuu wa 2015 umalizike na kufikia maazimio yafuatayo Kwa ajili ya maamuzi ya vikao vya chama.


  1. Chama kimeazimia kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uanze sasa Kwa kufanya marekebisho ya sheria ya kura ya maoni na sheria ya mchakato wa Katiba.


  Chama kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda timu ya wataalamu Kwa ajili ya kupita rasimu ya katiba ya Jaji Joseph Warioba na kuitisha Mkutano Mkuu wa kikatiba wa Wananchi ( National Constitutional Conference ) ili kupitisha katiba pendekezwa na kwenda kwenye Kura za maoni.

  Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeazimia kwamba iwapo Serikali itaamua kwenda na katiba pendekezwa iliyopo sasa itaipinga Kwa kufanya kampeni za HAPANA kwenye kura ya maoni.


  2. Wakati mchakato wa Katiba ukiwa umesimama Baraza la Wawakilishi la Zanzibar limepitisha sheria ya kutafuta mafuta na gesi kinyume na matakwa ya Katiba ya Muungano ambapo mafuta na gesi ni masuala ya Muungano.


  Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeshauri kuwa Chama kimwelekeze Mbunge wake ndani ya Bunge la Muungano kuwasilisha muswada binafsi wa Mbunge wa kufanya mabadiliko ya katiba ya Muungano Kwa kuondoa mafuta Na gesi Kama jambo la muungano ili kuiwezesha Zanzibar kuendelea na utafutaji Na uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia bila vikwazo vya kiufundi kwa ajili ya kikatiba.


  3. Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia umeazimia kwamba Chama kifanye maadhimisho ya miaka 50 ya Azimio la Arusha Mwezi Februari mwaka 2017 Kwa kufanya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha Na kutanguliwa na Halmashauri Kuu ya chama kwenye ukumbi ule ule ambao Chama cha TANU kilifanya Mkutano uliozaa Azimio la Arusha mwaka 1967.


  Imeshauriwa kuwa Wataalamu mbalimbali wa ndani na Nje ya nchi ya waalikwe kujadili mafanikio Na changamoto za Azimio la Arusha katika miaka 25 ya kutekelezwa kwake na madhara yake tangu lizikwe huko Zanzibar mwaka 1992

  Abdallah Khamis

  Afisa Habari ACT Wazalendo

  09/10/2016

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku