• Breaking News

  Oct 20, 2016

  Agizo la Waziri wa Elimu Prof Ndalichako Kwa Bodi ya Mikopo Kuhusu Mikopo ya Wanafunzi

  Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wa kutoa fedha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

  Waziri wa Elimu ameyasema hayo leo usiku wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa TBC ambapo amekiri kuwepo kwa mapungufu katika namna ya fedha hizo zinavyotolewa hali inayopelekea wanafunzi kupata fedha kidogo ambazo hazikidhi mahitaji.  Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sitofahamu kubwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku wengine wakipewa fedha kiasi kidogo ambazo hazitoshi kujikimu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku