Oct 8, 2016

AIR Tanzania ina Nafasi Nzuri Kushinda soko la Abiria wa Ndani

Leo niliamua kufanya booking ya safari ya ndege kutoka Mwanza kwenda Dar, safari ifanyike wiki moja kutoka sasa tarehe 15 octoba 2016.

Niliamua kuangalia na kulinganisha gharama za safari katika mashirika matatu tofauti yanayotoa huduma ya usafiri wa ndege ndani ya Tanzania. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

Air Tanzania
15 octoba 2016
Mwanza-Dar
Muda wa safari saa moja na nusu (1hr30Minutes)
Nauli jumla pamoja na kodi na mzigo kg 20= 180,000/


Fastjet
15 octoba 2016
Mwanza-Dar
Muda wa safari saa moja na dakika 35 (1hr35Minutes)
Nauli jumla pamoja na kodi na mzigo = 420,000/

Precision Air
15 octoba 2016
Mwanza-Dar
Muda wa safari masaa 2 dakika 10 (2hr10Minutes)
Nauli jumla pamoja na kodi = 415,380/


Mtazamo wangu,
Ikiwa hali hii itaendelea itaendelea basi Air Tanzania wana nafasi kubwa sana ya kuteka soko la ndani. Lakini hiyo itategemea pia na ubora wa huduma zao ndani na nje ya ndege. Hata hivyo kwa safari zinazohitaji booking ya mapema zaidi kama mwezi au miezi bila shaka Fastjet ataendelea kutamba. Kwa upande wa muda wa safari nimeshangaa kuwa Air Tanzania yuko vizuri zaidi.....cha msingi watende sawasawa na wasemacho, isiwe muda wa kwenye maandishi tu halafu uhalisia unakuwa tofauti kabisa.

Kila la kheri Air Tanzania...see you soon!!

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR