• Breaking News

  Oct 23, 2016

  Argentina yaongoza orodha ya FIFA ya timu bora duniani

  Shirikisho la soka duniani (FIFA) imetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka duniani, bado vinara wamesalia kuwa Argentina.

  Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.

  Tanzania inashika Nafasi ya 144 baada ya kuporomoka nafasi 12. Uganda wao wapo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107.

  Ethiopia wamo nafasi ya 126, Malawi 100 na Burundi 138.

  Nchi ambayo ipo juu kabisa kwa Bara la Afrika ni Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio nafasi ya 31 wakifuatiwa na Senegal ambao ni wa 32.

  Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24.

  Haya ni mataifa 10 bora duniani

  1.Argentina

  2.Ujerumani

  3.Brazil

  4.Ubelgiji

  5.Colombia

  6.Chile

  7.Ufaransa

  8.Ureno

  9.Uruguay

  10.Uhispania

  Mataifa 10 bora Afrika

  31 Ivory Coast

  32 Senegal

  35 Algeria

  38 Tunisia

  45 Ghana

  46 Misri

  49 DR Congo

  58 Mali

  59 Cameroon

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku