Oct 7, 2016

BABA Mrisho Ngassa Kocha mpya wa Toto


Baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Toto Africans, Rogasian Kaijage kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, uongozi wa Toto umemkabidhi mikoba hiyo kwa muda Khalifani Ngassa ili kusaidiana na Wajerumani waliopo katika benchi la ufundi la timu hiyo kabla ya kupata kocha mkuu mpya.


Katika michezo saba ambayo Kaijage aliiongoza timu hiyo, Toto imeshinda mechi moja, sare mbili na kufungwa mechi nne jambo ambalo liliinua hasira za mashabiki wa timu hiyo na kumlazimisha ajiuzulu kuinoa timu hiyo.


Kuhusu suala hilo la Khalfani ambaye ni baba mzazi wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, Mwenyekiti wa Toto, Godwin Aiko alisema: “Ni kweli tumeamua kumchagua Khalfani kuwa kocha wa muda.”


Alipotafutwa Khalfani alisema: “Kweli lakini mimi nitakuwa kocha wa muda tu wakati mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

1 comment:

  1. Wamekutafuta wenyewe?Au kulikuwa na namna mpaka wakakuchagua wewe,maana timu ikiendelea kufanya vibaya ujiandae na lawama kitu ambacho hatutaki kitokee kwako mzee wetu.

    ReplyDelete

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR