• Breaking News

  Oct 8, 2016

  Benki Zadaiwa Kusitisha Mikopo kwa Watumishi wa Umma Kwa Muda Usiojulikana!

  Benki zimesitisha kutoa mikopo kwa watumishi wa umma hasa waalimu kwa kigezo cha uhakiki unaondelea!

  Jambo la ajabu ni kwamba uhakiki huu umeanza tangu January mwaka huu na serikali imetangaza kupitia mh rais kuwa wamegundua zaidi ya wafanyakazi hewa 17000 lakini hadi leo tunaambiwa uhakiki unaendelea.

  Hili tayari limeshaleta madhara kwa wengi kwani licha ya kusitishwa ajira mpya na kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi, hata kukopa benki imekuwa ishu.

  Hii si haki kwa watumishi wa umma na ni aina fulani ya unyanyasaji!

  Uhakiki huu umechukua muda mrefu kupitiliza kwani watumishi wa umma hawazidi milioni moja kwa sensa ya mwsks 2012. Sasa iweje ichukue mwaka mmoja kuhakiki watu milioni 1 huku haki zao mbalimbali zikiminywa?

  Mikopo ya benki huwa haitolewi kinyemela, lazima taasisi husika na benki wajiridhishe kuwa anayekopa kweli ni mtumishi wa umma. Huwezi kupewa mkopo bila kupewa go ahead na mwajiri wako na benki kujiridhisha hivyo!

  Tafadhali serikali tunaomba jitihada zenu za kuziba mianya ya wizi ktk utumishi wa umma zisiwakosehe au kuwa kikwazo katika maendeleo ya watumishi kiuchumi. Hii inatuua morali ya kazi kabisa!

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku