• Breaking News

  Oct 31, 2016

  Bondia Thomas Mashali Auawa Kwa Kipigo, Adaiwa Kuitiwa Kelele za Mwizi


  Bondia Thomas Mashali ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa na watu baada ya kudaiwa kuitiwa kelele za mwizi, kwa mujibu wa taarifa ya mtu wake wa karibu.

  Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.

  Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi.

  Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta. Inasemekana kuwa hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

  Habari zaidi zitakujia punde.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku