Oct 2, 2016

BREAKING News: Kocha Julio Aamua Kujiuzulu Ukocha


Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Mwadui inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Jamhuri Kihwelu amesema huenda akaacha kufundisha mpira kwa madai ya timu yake kuonewa na waamuzi.

Julio ametoa kauli hiyo mara ya baada ya kumalizika kwa mchezo wa timu yake dhidi ya Mbeya City FC, mchezo uliopigwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya na kushuhudia Mwadui ikipigwa bao 1-0, likifungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 33 ya mchezo.

Julio amesema waamuzi wan chi hii ndiyo wanaokwamisha mpira, huku akimlalamikia mwamuzi wa mchezo wa leo kwa kuwanyima nafasi nyingi za faul, na kuongeza kuwa hawezi kuendelea kulalamika kila siku juu ya waamuzi huku akitumia nguvu nyingi na gharama kubwa kuandaa timu.

Kwa matokeo hayo, Mwadui ambayo msimu huu imeonekana kuanza vibaya ikilinganishwa na msimu uliopita, imebaki na point zake 5, kwa kushinda mechi moja, droo 2 na kupoteza michezo mine kati ya 7 iliyocheza.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR