Habari zilizoifikia ambazo hazijathibishwa na TFF, Bodo ya ligi wala chama cha waamuzi ni kwamba, mwamuzi wa kati Martin Saanya na msaidizi wake namba moja (line one) Samwel Mpenzu, wamefungiwa miaka miwili kuchezesha soka.

Chanzo chetu kimeitutonya kuwa, uamuzi huo umefikiwa na kamati ya saa 72 iliyokutana kuwajadili wawili hao baada ya kuwepo kwa malalamiko kwenye mechi ya Yanga vs Simba waliyoichezesha Jumamosi October 1.

“Martin Saanya na Samwel Mpenzu wamefungiwa miaka miwili lakini line two Ferdinand Chacha yeye amesalimika,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutoandikwa jina.

“Kadi nyekundu aliyooneshwa Jonas Mkude imefutwa baada ya kamai hiyo kujiridhisha kuwa kadi hiyo ilitolewa kimakosa.”

Baada ya mchezo wa Yanga vs Simba, kuliibuka mijadala mingi na mikubwa juu ya mwamuzi Martin Saanya kulikubali goli la Tambwe ambaye aliushika mpira kabla hajafunga huku Samwel Mpenzu akilaumiwa kwa kulikataa goli la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa madai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako ili Kupata Habari zetu Haraka


POST A COMMENT

Post a Comment

 
Top