• Breaking News

  Oct 28, 2016

  Breaking News: Mwigulu Nchemba Amrejesha Kocha Hans Van Der Pluijm Yanga


  Mh. Mwigulu Nchemba amemrejesha kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyo mapema wiki hii.

  Katika mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.

  Hii ni mara ya pili Mwigulu Nchemba anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya Club ya Yanga,msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha Kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.
  Ikumbukwe,Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchini na mpenzi wa Soka na Mwanachama wa Jangwani "Yanga" #Regrann

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku