Oct 18, 2016

Bushoke Asema Utendaji wa Rais Magufuli Umekuwa Gumzo Afrika Kusini

Msanii wa muziki ambaye amekuwa akiishi nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu, Bushoke amefunguka kwa kusema kuwa kama kuna mtu ambaye ni gumzo nchini Afrika Kusini basi ni Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, kutokana na maamuzi magumu katika utendaji kazi zake na kuwa muwazi.

Muimbaji huyo amesema magazeti makubwa nchini humo yamekuwa yakiandika kuhusu utendaji mzuri wa Rais huyo huku wakimtaka Rais Zuma kuiga utendaji wake.

“Nilisoma gazeti moja la Afrika Kusini linaloitwa ‘Sowetan’ lilikuwa na kichwa cha habari kinachosema Jacob Zuma ‘can not do like Magufuli, lakini ndani walielezea vitu ambavyo amefanya Magufuli na Zuma hawezi kuvifanya, hivyo anazungumziwa kama mtu mashuhuri,” Bushoke aliliambia gazeti la Mwanaspoti.

Pia mkali huyo anafichua kuwa, mbali na JPM, mtu mwingine anayetajwa sana Sauzi na kuwa gumzo kubwa ukimuondoa pia Diamond ni mwanadada Vanessa Mdee ‘Vee Money.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR