Oct 24, 2016

CCM Yajipanga Kumvua Uanachama Diwani wa Sambasha Baada ya Kujifanya Usalama wa Taifa

Lengai ole Sabaya 
Wakazi wa Kata ya Sambasha wilayani Arumeru wanaweza kukosa mwakilishi kwenye baraza la madiwani iwapo mpango wa CCM Mkoa wa Arusha wa kumvua uanachama diwani wao, Lengai ole Sabaya utatekelezwa.

Akizungumza kwa simu kuhusu mpango wa kuvuliwa uanachama, Sabaya alisema hakuna mwenye mamlaka kisheria ya kufanya hivyo na iwapo hilo litafanyika anasubiri uamuzi huo.

CCM inajipanga kumvua uanachama Sabaya ambaye pia alisimamishwa uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani hapa kwa tuhuma za kukiuka maadili.

Hivi karibuni Sabaya alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha na kusomewa mashtaka ya kujifanya ofisa usalama wa Taifa na kughushi kitambulisho cha ofisi hiyo. Yuko nje kwa dhamana.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR