• Breaking News

  Oct 23, 2016

  CCM Yashinda Uchaguzi wa Meya Kinondoni..Ukawa Wasusa

  Uchaguzi wa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umefanyika le ambapo Benjamin Sitta amechaguliwa kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa jumla ya kura 18, huku George Manyam akichaguliwa kuwa Naibu Meya.

  Washindi wote ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani awali Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilisusia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM imeongeza wajumbe wa kupiga kura kinyemela na hivyo mgombea wao kupa kura 0.

  Uchaguzi wa Manispaa hiyo umefanyika tena baada ya manispaa hiyo kugawanywa na kuunda manispaa mbili kufuatia kuundwa kwa Wilaya mpya wa Ubungo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku